Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeendelea kuwekeza katika kuinua ustawi na mazingira bora ya timu za taifa baada ya kusaini mkataba mkubwa wa udhamini wa miaka miwili na kampuni ya Watercom Tanzania.
Katika hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam, Rais wa TFF Bw. Wallace Karia na Meneja Masoko wa Watercom Bw. Mohamed Salim walisaini makubaliano yanayohusisha udhamini wa vinywaji rasmi vitakavyotumika katika programu zote za timu za taifa ikiwemo maji safi ya kunywa na juisi za kuongeza nguvu.
Kwa mujibu wa makubaliano hayo, Watercom itahakikisha timu zote za taifa zikiwemo Serengeti Boys, Twiga Stars, Taifa Stars na timu nyingine kwenye ngazi mbalimbali zin