
1.Utangulizi
Tamasha la Michezo kwa wanawake (Tanzanite Women Sports Festival) lillianzishwa kutokana na historia kuonesha kuwa nchini Tanzania pamoja na ushiriki wa wanawake wachache katika michezo, wanawake hao wamekuwa wakifanya vizuri na kuliletea Taifa sifa. Tamasha hilo limeweza kufanyika mwaka 2021, 2022, 2023 na 2025 na hufanyika kwa kuandaliwa matukio kama; Kongamano lenye mafunzo mbalimbali kwa wanawake, utoaji wa tuzo za heshima kwa wanawake waliofanya vizuri katika michezo pamoja na mashindano ya michezo mbalimbali inayohusu wanawake kama netiboli, mpira wa miguu wanawake, rede, mpira wa wavu, mpira wa kikapu na karate. Matukio haya yamekuwa yakifanyika katika miaka tofauti tofauti wakati wa mashindano hayo. Washiriki ni viongozi wanawake wa Michezo, Maafisa Michezo wanawake wa Wilaya na Mikoa, Watumishi wanawake wa Wizara na Baraza na wadau wa michezo wanawake.
2.Chimbuko la Tamasha la Tanzanite
Chimbuko la Tamasha la Tanzanite ni maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kipindi alichokuwa anawapongeza wanawake waliofanya vizuri katika michezo alitoa maelekezo kwa Wizara kufanya jambo ili kuenzi ushiriki wa wanawake katika michezo na ndipo likaanzishwa tamasha la tanzanite linalobeba “theme” ya “Celebrating the power of women in sports”
3.Lengo la Tamasha la Tanzanite
Lengo kuu la Tamasha la michezo kwa wanawake ni kuhamasisha ushiriki wa wanawake katika michezo na kuenzi juhudi za wanawake waliofanya vizuri katika Sekta ya Michezo.
4.Kamati ya Maandalizi ya Tamasha
Katika kuhakikisha Tamasha linafanyika iliteuliwa na Mheshimiwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Kamati maalum ya kuratibu maandalizi ya Tamasha hilo inayoongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo ni Bi. Neema Y. Msitha Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa. Wafuatao ni wajumbe wa kamati ya maandalizi ya tamasha la michezo kwa wanawake;
|
Na. |
Jina |
Taasisi Anayotoka |
Simu |
|
1. |
Neema Y. Msitha |
BMT |
0683252572 |
|
2. |
Christina Luambano |
WUSM |
0712913831 |
|
3. |
Leah Kihimbi |
WUSM |
0784364206 |
|
4. |
Dkt. Devotha Marwa |
UDSM |
0754311419 |
|
5. |
Nasriya Nassor |
Zanzibar |
0773032111 |
|
6. |
Nasra Mohamed |
Zanzibar |
0777416778 |
|
7. |
Rehema Mwendo |
CLOUDS FM |
0712608022 |
|
8. |
Irene Mwasanga |
TOC |
0784619435 |
5. Mafanikio
Kuhamasisha wanawake kushiriki katika michezo pamoja na kuhamasisha kushika nafasi za uongozi katika michezo
Timu ya Taifa ya Kuogelea Tanzania iliyokuwa na jumla ya wan...
Tanzania imeandika historia mpya katika mchezo wa kikapu kwa...
Timu ya Taifa ya Wavulana chini ya umri wa miaka 15 (U15) in...
Shirikisho la Mchezo wa Karate Nchini Tanzania (TSKF) lime...
Timu za mpira wa mikono za Ngome kwa wanaume na wanawake zim...