TANZANIA U 15 KUIANZA KAMPENI YA KOMBE LA DUNIA DH...

TANZANIA U 15 KUIANZA KAMPENI YA KOMBE LA DUNIA DHIDI YA ZAMBIA

23 Oct, 2026
TANZANIA U 15 KUIANZA KAMPENI YA KOMBE LA DUNIA DHIDI YA ZAMBIA

Timu ya Taifa ya Wavulana chini ya umri wa miaka 15 (U15) inatarajiwa kuanza kampeni yake katika Tamasha na Kombe la Dunia la FIFA U15 kwa kucheza dhidi ya Zambia, Oktoba 24, 2026, jijini Baku, nchini Azerbaijan.

Kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu Mohamed Amin kimewasili salama nchini Azerbaijan na kinajiandaa kwa mchezo huo wa kwanza, huku kikiwa na lengo la kufanya vizuri katika mashindano hayo ya kimataifa.

Tanzania imepangwa Kundi X pamoja na Zambia, Uruguay, Comoros, Moldova na Montenegro, ambapo timu hizo zitachuana katika hatua ya makundi kabla ya kuingia hatua zinazofuata za mashindano kulingana na matokeo yao.

Kwa mujibu wa ratiba, baada ya kukutana na Zambia, Tanzania itacheza michezo miwili Oktoba 25 dhidi ya Comoros na Montenegro, kabla ya kumaliza hatua ya makundi Oktoba 26 kwa kukabiliana na Uruguay na Moldova.

Mashindano hayo yanayoanza Oktoba 24 hadi 30, 2026, ni fursa muhimu kwa vijana wa Tanzania kupata uzoefu wa kimataifa, kuonyesha vipaji vyao na kujiendeleza kupitia ushindani na timu kutoka mataifa mbalimbali duniani.

Caption