TIMU YA TAIFA YA KUOGELEA TANZANIA YANG’ARA MASHIN...

TIMU YA TAIFA YA KUOGELEA TANZANIA YANG’ARA MASHINDANO YA KUOGELEA YA KANDA YA TATU AFRIKA NCHINI UGANDA

26 Oct, 2026
TIMU YA TAIFA YA KUOGELEA TANZANIA YANG’ARA MASHINDANO YA KUOGELEA YA KANDA YA TATU AFRIKA NCHINI UGANDA

Timu ya Taifa ya Kuogelea Tanzania iliyokuwa na jumla ya wanamichezo 35, imefanya vizuri katika Mashindano ya Kuogelea ya Kanda ya Tatu Afrika yaliyofanyika nchini Uganda, kwa kushika nafasi ya tatu katika matokeo ya jumla ya mashindano hayo.

Aidha, timu hiyo imeshika nafasi ya tatu katika mashindano ya kuogelea kwenye maji ya wazi (Open Water), na hivyo kuendeleza mafanikio ya Tanzania katika mashindano hayo.

Kwa ujumla, timu imefanikiwa kutwaa vikombe nane na kupata jumla ya medali 85, zikiwemo medali za dhahabu 24, fedha 29 na shaba 32.

Katika mchezo wa Water Polo, timu ya Tanzania ya vijana wadogo (Junior) nayo imefanya vizuri kwa kushika nafasi ya tatu na kutwaa kikombe cha mshindi wa tatu.

Caption