Sisi ni nani
Baraza la Michezo la Taifa (BMT) ni Taasisi ya serikali iliyoundwa na Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kwa sheria Na. 12 ya mwaka 1967 na marekebisho yake ya sheria Na.6 ya mwaka 1971 na Kanuni za Baraza la Michezo la Taifa na Kanuni za usajili Na.442 za mwaka 1999 na ndio chombo pekee kilichopewa mamlaka na Bunge kusimamia Michezo nchini. Aidha Baraza la Michezo la Taifa ni Taasisi iliyopo chini ya Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo.