Sisi ni nani

 

Baraza la Michezo la Taifa (BMT) ni Taasisi ya Serikali  iliyoundwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Sheria Na.12 ya Mwaka 1967 na Marekebisho yake Na. 6 ya 1971 na No. 3 ya 2018 ya Baraza la Michezo la Taifa. Baraza la Michezo la Taifa limepewa jukumu la kusimamia michezo yote  Tanzania.

 

“DIRA”

” Kuwa na Taifa lenye watu wenye Afya, wakakamavu na ufanisi kwenye michezo kwa maendeleo ya jamii, umoja na taifa

“DHAMIRA”

” Kutoa fursa sawa ya ushiriki kwa watu wote katika michezo ili kuongeza ufanisi”

MAJUKUMU YA BARAZA LA MICHEZO LA TAIFA

  • Kuendeleza, kustawisha na kudhibiti aina zote za Michezo kitaifa kwa ushirikiano na vyama au vikundi vya michezo
  • Kuhimiza na kutoa fursa za ushirikiano miongoni mwa vyama mbalimbali vya Taifa.
  • Kuidhinisha mashindano ya kitaifa na ya kimataifa katika michezo na matamasha yaliyoandaliwa na vyama vya kitaifa na vyama vingine.
  • Kupanga kwa kushirikiana na serikali za mitaa kwa ajili ya kutenga maeneo kwa ajili ya michezo.
  • Kuhamasisha ushiriki wa jamii katika michezo.
  • Kupanga na kuishauri Wizara yenye dhamana ya Michezo juu sera ya ukuzaji wa michezo nchini.