TOZO ZA BMT

Katika Kusimamia na Kuratibu Michezo nchini Baraza la Michezo linatoa huduma mbalimbali kwa gharama na tozo  zifuatazo:- 

S/no

KIFUNGU

MAELEZO YA TOZO

MAELEZO YA TOZO

KIWANGO CHA TOZO

1 21(3)(b) Gawio kutoka katika mikataba ya udhamini na haki za matangazo ya television Itatolewa na vilabu, vyama, mashirikisho au taasisi zinazodhaminiwa 1% ya thamani ya mkataba wa udhamini
2 24(1) na (3) Rufaa Rufaa kwenda Kamati za Michezo za Wilaya, Mikoa, Baraza na Waziri Hakuna tozo 
3 24(1) na (3) Rufaa Rufaa kwenda katika vyama vya michezo Kiwango kitapangwa kwa mujibu wa katiba ya vyama husika. 
4 30(2) Kuwasilisha mapato kwa Baraza endapo mchezo umeshuhudiwa bila kiingilio Itatolewa na mtu, klabu, chama au shirikisho lililodhamini watazamaji kuingia bila kiingilio katika mchezo husika 500,000/= 
5 30(3) Faini ya kutowasilisha mapato ya Baraza kwa wakati.  Inalipwa na chama kilichokiuka kupeleka mapato ya Baraza kwa wakati.  1% ya fedha ambayo haijawasilishwa. 
6 31(7)(b) Faini ya kukiuka masharti ya kuajiri mchezaji au mtaalamu kutoka nje ya Tanzania Italipwa na klabu, chama au shirikisho lililokiuka USD 500
7 33(4) Uhakiki wa mikataba ya udhamini na Matangazo ya Televisheni Uhakiki utaombwa na anayedhaminiwa 1% ya mapato yatokanayo na mikataba husika. 
8 33(4) Faini ya kukiuka uhakiki wa mikataba ya udhamini na matangazo ya televisheni.  Itatozwa kwa klabu, chama, shirikisho au Taasisi iliyodhaminiwa.  2% ya thamani ya mkataba
9 34(3) Uhakiki wa mikataba ya udhamini na matangazo ya timu za Taifa Itawasilishwa na chama kinachodhaminiwa Hakuna Tozo.