Kusimamia na Kuratibu Michezo

Katika kusimamia na kuratatibu michezo Baraza linatekeleza kazi zifuatazo:- 

i.  Kuendeleza, kustawisha na  kudhibiti aina zote za michezo ya Ridhaa Kitaifa kwa ushirikiano na Vyama au Vikundi vya Michezo vya  Ridhaa ya Hiari kwa kutoa:-

 a. Mafunzo na watumishi  wengine.

 b. Misaada kwa Vyama au Vikundi vya Kitaifa;

 c. Viwanja vya Michezo na fursa nyinginezo;

 d. Vifaa vya michezo na vitu  vingine ambavyo ni muhimu kwa ajili ya kuendeleza michezo

ii. Kuidhinisha mashindano ya Taifa na ya Kimataifa katika michezo na  Tamasha vilivyoandaliwa na Vyama vya Taifa na Vyama vingine.

iii. Kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu maswala ya michezo na ufundi 

iv. Kuandaa baada ya kushauriana na Vyama vya Taifa vinavyohusika,  Mashindano na Tamasha vya Kitaifa na Kimataifa kwa nia ya kubadilishana uzoefu na kukuza mahusiano ya

Kirafiki na mataifa mengine.

v. Kuhimiza na kutoa fursa za Ushirikiano miongoni mwa Vyama mbalimbali vya Taifa;

vi. Kusimamia na kuratibu chaguz za Vyama/ Mashirikisho ya Michezo ili kupata viongozi bora. 

vii. Kuamsha ari ya kupenda aina zote za michezo kwa ngazi zote na;

viii. Kutunga Sera ya ukuzaji michezo