Vibali vya Michezo

Sheria ya Baraza la Michezo la Taifa Sura No. 49, Kanuni zimetengenzwa chini ya Kifungu cha 28, Kanuni ya marekebisho ya Baraza la Michezo la Taifa za Mwaka 2020. 

Baraza la Michezo la Taifa ndilo lenye mamlaka ya Kuratibu vibali mbalimbali vya michezo nchini. Vibali vinavyotolewa na Baraza la Michezo ni kama ifutavyo:- 

i. Kifungu 17(1) na (2) Kibali cha kwenda nje ya nchi au kuingia nchini Tanzania kwa ajili ya michezo ya kimataifa

Mchanguo wa gharama za Kupata vibali hivyo ni kama ifuatavyo:- 

S/NO AINA YA KIBALI KIWANGO CHA TOZO
1 Kibali cha kwenda kufanya tukio nje ya nchi au kuingia kufanya michezo nchini kwa vilabu vya kulipwa 200,000/=
2 Kibali cha kwenda kufanya tukio nje ya nchi kwa mwanamichezo wa kulipwa 50,000/=
3 Kibali cha kwenda kufanya tukio nje ya nchi au kuingia nchini kwa ajili ya kufanya michezo kwa vyama na vilabu vya ridhaa  20,000/=
4 Vibali kwa ajili ya wanamichezo wanaoenda kwenye mashindano, matamasha au mabonanza ya Taasisi za serikali, timu za Taifa, michezo ya wenye ulemavu.  Hakuna Tozo

 

ii. Kifungu 25 (3) Kibali cha kuandaa matukio ya michezo kwa wakuzaji na mawakala wa ndani.

Mchanguo wa gharama za Kupata vibali hivyo ni kama ifuatavyo:- 

S/NO AINA YA KIBALI KIWANGO CHA TOZO
1 Kibali cha kuandaa mbio za marathoni na mbio nyingine za barabarani za kimataifa hapa nchini 1,000,000/= 
2 Kibali cha kuandaa mbio za marathoni na mbio nyingine za kitaifa hapa nchini  500,000/=
3 Kibali cha matukio mengine ya michezo ya kimataifa ambayo siyo marathoni  200,000/=
4 Kibali cha matukio mengine ya michezo ya kitaifa ambayo siyo marathoni 100,000/=
5 Kibali cha kuandaa matukio ya Michezo kwa wakuzaji au wakala kutoka nje ya Tanzania (Maombi yatawasilishwa na mwenyeji wao)  USD 500

 

iv. Kifungu 31(2)(c)  Kibali na idhini ya kuajiri mchezaji au mtaalamu wa michezo kutoka nje ya nchi 

S/NO AINA YA KIBALI MAELEZO YA KIBALI KIWANGO CHA TOZO
1 Maombi ya idhini ya kuajiri mchezaji au mtaalamu wa michezo kutoka nje ya nchi  Idhini itaombwa na klabu, chama au shirikisho linalomuajiri USD 500

 

v. Kifungu 31(6) Maombi ya idhini ya kuajiri mchezaji au mtaalam kutoka nje ya Tanzania kwa klabu ambayo haikumleta. 

S/NO AINA YA KIBALI MAELEZO YA KIBALI KIWANGO CHA TOZO
1 Maombi ya idhini ya kuajiri mchezaji au mtaalamu kutoka nje ya Tanzania kwa klabu ambayo haikumleta nchini idhini itaombwa na klabu, chama, shirikisho linalomchukua baada ya kuwa ameshindwa kukubaliana au amemaliza mkataba wake na klabu, chama au shirikisho la awali  USD 500