ZIARA VIWANJA VYA MICHEZO
service image
10 May, 2025

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Paramagamba Kabudi amewataka Wakandarasi wanaofanya marekebisho katika dimba la Benjamini Mkapa,Shule ya Sheria na uwanja wa Gymkhana waharakishe ili viwanja hivyo viwe tayari kwaajili ya mashindano ya CHAN 2024 yatakayofanyika Kenya, Uganda na Tanzania Agosti mwaka huu .

Hayo ameyasema leo alipofanya ziara maalumu akiongozana na Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa kwenye viwanja hivyo jijini Dar es salaam na kuongezea kuwa Uwanja wa Benjamini Mkapa mpaka sasa kwenye ukarabati umefiki asilimia 85.

" Tumeanza na kiwanja shule ya Sheria vyumba vya kubadilishia nguo umekamilika vimebaki mambo machache lakini ujenzi wa wavu wakuzuia mpira huku changamoto kubwa tuliyokuwa nayo ilikuwa ni (Pitch) kiwanja cha kuchezea viwanja hivi sio viwanja vya nyasi bandia au nyasi chotara ni vya nyasi asilia ambayo inahitaji utaalamu wa hali ya juu,kujua haina ya udongo ulionao aina ya maji yanayopatikana lakini pia kama unavyoona ni lazma kujua aina ya majani yanayopaswa kuwa pale.

"Kazi hiyo ya kutusaidia katika uwanja tumeipa kampuni ya uturuki ya Reform Sports ambao wao wanauzoefu mkubwa tu wa kujenga viwanja na wamefanya kazi hii katika nchi 160 na hapa Afrika Tanzania ni nchi ya 16 na tayari wamefanya kazi kubwa kule Zanzibar kwahiyo tulipoona tuna changamoto hii tuliona tuwatumie wataalamu na toka wameanza hawajamaliza mwezi na tumeona maendeleo makubwa tunahakika mpaka mwezi Mei vile viwanja vya mazoezi vya Shule ya Sheria na Gymkhana vitakuwa vishakamilika" Amesema Kabudi

Aidha Kabudi amesema mchezo wa fainali kati ya Simba dhidi ya RS Berkane utachezwa katika uwanja wa Benjamini Mkapa na yale yote Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) waliyoyowaletea ili wawe wameyakamilisha yamekamilika

"Kazi nyingine kubwa ambayo ilikuwa inafanyika hapa ni. kubadili viti mpaka sasa tunaona kazi ya kubadili viti inaenda vizuri tumekwisha badilisha viti 38,000 kwahiyo ndani ya muda mfupi eneo hili litakuwa limejaa viti, 20,000 vimeshaagizwa vipo njiani tunatarajia vifike tarehe 15 ya mwezi huu baada ya hapo kazi ya kufunga itakuwa imekamilika.