Mbio za wanawake
PROGRAMU YA MASHINDANO YA “LADIES FIRST”
Mashindano ya Riadha ya Wanawake “Ladies First” yanaratibiwa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kwa kushirikiana na Taasisi ya Ushirikiano wa Kimataifa ya Japan hufanyika kila mwaka tangu mwaka 2019 ambapo mwaka 2026 utakuwa ni msimu wake wa nane. Mashindano haya yamekua yakifanyika Jijini Dar es Salaam. Programu hii inatambulika na Serikali kupitia Kamati za Michezo za Mikoa, Wilaya na Shirikisho la Riadha Tanzania (RT).
Lengo la mashindano hayo ni kuibua, kukuza na kuendeleza vipaji vya wana michezo wanawake katika kushiriki mchezo wa riadha.
Michezo wanayoshiriki ni mbio fupi, mbio za kati na mbio ndefu, miruko, na mirusho ambapo katika mirusho hurusha mkuki pekee.
Mashindano haya ni endelevu kwani ni mpango wa kudumu ambao unaratibiwa kuendelea kukuza vipaji vya wanamichezo ili kupata wanariadha wanawake mahiri watakaowakilisha nchi katika mashindano ya kitaifa na kimataifa.
Programu hii umesaidia kuibua na kuendeleza vipaji vya wanariadha maarufu nchini kama Magdalena Shauri, Jackline Sakilu, Angela John pia umesaidia kuhamasisha wanawake wengi kushiriki michezo nchini kuanzia ngazi ya vijijini.
Mpango huu upo chini ya mpango wa baraza la michezo la taifa sambamba na mpango wa taifa wa kuhakikisha tunahamasisha jamii yote kushiriki michezo wakiwemo wanawake.
Programu hii inadhaminiwa na Shirika la Maendeleo la Japan (JICA) na washirika wengine.

