TVF YAJIPANGA KUENDELEZA MASHINDANO YA MPIRA WA WAVU UFUKWENI
service image
26 May, 2026

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Wavu Tanzania (TVF), Laurance Safari amesema mashindano ya Mpira wa Wavu Ufukweni Afrika Kanda ya Tano yaliyohitimishwa Mei 25, 2026 katika Fukwe ya Sawa Sawa jijini Dar es Salaam yamekuwa na manufaa makubwa kwa Tanzania katika kujifunza maandalizi na uendeshaji wa mashindano ya mchezo huo.

Ameeleza kuwa uwepo wa washiriki kutoka mataifa mbalimbali umeongeza undugu, ushirikiano na urafiki mkubwa katika kipindi chote cha mashindano hayo, jambo lililosaidia kukuza mahusiano ya kimichezo ndani ya ukanda huo.

Aidha, Laurance Safari amesema TVF ina mpango wa kuanzisha mashindano ya mpira wa wavu ufukweni yatakayokuwa yakifanyika kila mwisho wa mwezi katika Fukwe za Coco jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuendelea kuukuza mchezo huo nchini.

“Shirikisho lina mpango wa kuanzisha mashindano ya wavu wa ufukweni yatakayokuwa yakifanyika kila mwisho wa mwezi katika Fukwe za Coco jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuendelea kukuza mchezo,” amesema Safari.

Hatua hiyo inatajwa kuwa sehemu ya mikakati ya TVF ya kuongeza ushindani, kuibua vipaji na kuendeleza mchezo wa mpira wa wavu ufukweni nchini Tanzania.

slot gacor