Tamasha la Michezo la wanawake

TAMASHA LA MICHEZO LA WANAWAKE

  1. Utangulizi

Tamasha la Michezo kwa wanawake (Tanzanite Women Sports Festival) lillianzishwa kutokana na historia kuonesha kuwa nchini Tanzania pamoja na ushiriki wa wanawake wachache katika michezo, wanawake hao wamekuwa wakifanya vizuri na kuliletea Taifa sifa. Tamasha hilo limeweza kufanyika mwaka 2021, 2022, 2023 na 2025 na hufanyika kwa kuandaliwa matukio kama; Kongamano lenye mafunzo mbalimbali kwa wanawake, utoaji wa tuzo za heshima kwa wanawake waliofanya vizuri katika michezo pamoja na mashindano ya michezo mbalimbali inayohusu wanawake kama netiboli, mpira wa miguu wanawake, rede, mpira wa wavu, mpira wa kikapu na karate. Matukio haya yamekuwa yakifanyika katika miaka tofauti tofauti wakati wa mashindano hayo. Washiriki ni viongozi wanawake wa Michezo, Maafisa Michezo wanawake wa Wilaya na Mikoa, Watumishi wanawake wa Wizara na Baraza na wadau wa michezo wanawake.

  1. Chimbuko la Tamasha la Tanzanite

Chimbuko la Tamasha la Tanzanite ni maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kipindi alichokuwa anawapongeza wanawake waliofanya vizuri katika michezo alitoa maelekezo kwa Wizara kufanya jambo ili kuenzi ushiriki wa wanawake katika michezo na ndipo likaanzishwa tamasha la tanzanite linalobeba “theme” ya Celebrating the power of women in sports”

  1. Lengo la Tamasha la Tanzanite

Lengo kuu la Tamasha la michezo kwa wanawake ni kuhamasisha ushiriki wa wanawake katika michezo na kuenzi juhudi za wanawake waliofanya vizuri katika Sekta ya Michezo.

  1. Kamati ya Maandalizi ya Tamasha

Katika kuhakikisha Tamasha linafanyika iliteuliwa na Mheshimiwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Kamati maalum ya kuratibu maandalizi ya Tamasha hilo inayoongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo ni Bi. Neema Y. Msitha Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa. Wafuatao ni wajumbe wa kamati ya maandalizi ya tamasha la michezo kwa wanawake;

Na.

Jina

Taasisi Anayotoka

Simu

1.

Neema Y. Msitha

BMT

0683252572

2.

Christina Luambano

WUSM

0712913831

3.

Leah Kihimbi

WUSM

0784364206

4.

Dkt. Devotha Marwa

UDSM

0754311419

5.

Nasriya Nassor

Zanzibar

0773032111

6.

Nasra Mohamed

Zanzibar

0777416778

7.

Rehema Mwendo

CLOUDS FM

0712608022

8.

Irene Mwasanga

TOC

0784619435

 

  1. Mafanikio

Kuhamasisha wanawake kushiriki katika michezo pamoja na kuhamasisha kushika nafasi za uongozi katika michezo

  • Tamasha la Tanzanite limekuwa jukwaa la wanawake wanaofanya vizuri katika Sekta ya michezo kujitangaza na kujulikana zaidi
  • Wadau wa michezo wanawake kupata elimu ya ujasiliamali, namna ya kutafuta wadhamini na elimu ya masoko,
  • Kutoa vifaa vya michezo kwa shule (3) za kuibua na kuendeleza michezo Mkoani Arusha
  • Kutoa tuzo za heshima kwa wanawake waliofanya vizuri katika Sekta ya Michezo.