KAZI ZA BMT
MAJUKUMU YA BMT KAMA ILIVYOBAINISHWA NA SHERIA YA BMT Na. 12 ya 1967 NA KAMA ILIVYOBORESHWA NA SHERIA YA 1967 NI:
- Kuendeleza, kustawisha na kudhibiti aina zote za michezo ya ridhaa kwa kushirikiana na Vyama vya Michezo
- Kuhimiza na kutoa fursa na ushirikiano miongoni mwa Vyama vya michezo
- Kuidhinisha mashindano ya kitaifa na kimataifa ya michezo na matamasha yanayoandaliwa na Vyama vya michezo.
- Kuandaa baada ya kushauriana na Vyama vya michezo vinavyohusika mashindano ya kitaifa na kimataifa nia ikiwa ni kubadilishana uzoefu na kukuza mahusiano ya kirafiki na mataifa mengine.
- Kuamsha ari ya kupenda aina zote za michezo kwa ngazi zote.
- Kutoa baada ya kushauriana na vyama vya Taifa,Nishani, stashahada,vyeti,vikombe na vivutio vingine kwa ajili ya kuhimiza na kukuza shughuli za michezo
- Kudhamini nafasi za masomo kwa ajili ya mafunzo ya walimu wa michezo na waandaaji
- Kumshauri Waziri kuhusu mahusiano ya nje katika uwanja wa Michezo.
- Kushirikiana na mamlaka za serikali za mitaa ili kuwezesha kuwepo kwa fursa za michezo kwa ngazi zote na kujatahidi kujenga moyo wa uanamichezo na nidhamu kwa wanamichezo wote
- Kushauriana na vyama, taasisi au watu wengine kuhusiana na michezo ya ridhaa