BMT YAIMARISHA USHIRIKIANO WA MAENDELEO YA KRIKETI
Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Bi. Neema Msitha, amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Chama cha Kriketi Tanzania, Dkt. B.S. Free Kumar, pamoja na mkongwe wa mchezo wa kriketi kutoka India, Bw. Sandeep Patil Ji.
Mazungumzo hayo yalilenga kuimarisha ushirikiano na kubadilishana uzoefu katika kuendeleza na kukuza mchezo wa kriketi nchini.
Bi. Msitha alisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya wadau wa ndani na wa kimataifa katika kuimarisha maendeleo ya michezo wa kriketi nchini, huku akibainisha kuwa BMT itaendelea kushirikiana na wadau na vyama vya michezo vya kimataifa ili kuhakikisha michezo inakua na kufikia viwango vinavyotakiwa.
Aidha Bw. Sandeep na Dkt. Sree Kumar walieleza utayari wao wa kushirikiana na wadau wa michezo nchini katika kuendeleza kriketi kupitia kubadilishana uzoefu, mafunzo na programu za maendeleo ya mchezo wa kriketi nchini.

