BMT WAKUTANA NA HOTELI YA TIFFANY DIAMOND
29 Jan, 2026
Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Bi. Neema Msitha, leo tarehe 29 Januari, 2026, amekutana na mmoja mdau mkubwa wa michezo nchini, Hoteli ya Tiffany Diamond iliyopo jijini Dar es Salaam.
Lengo la kikao hicho ni kukuza na kuimarisha ushirikiano baina ya Baraza la Michezo la Taifa na wadau binafsi, hususan katika kuimarisha huduma kuelekea katika mashindano ya AFCON 2027
Ujumbe kutoka Hoteli ya Tiffany Diamond uliwakilishwa na Bi. Monica Magege, Mtendaji Mkuu wa Mauzo na Masoko, pamoja na Bw. Thomas Fusi, Meneja Msaidizi wa Mauzo na Masoko.

