KANUNI ZA USAJILI
“Baraza” maana yake ni Baraza la michezo la Taifa (BMT);
“Chama” maana yake ni Chama, Jumuiya, Kikundi au Klabu yoyote inayo jishughulisha na michezo:
“Kamati” maana yake ni kamati ya Michezo ya Mkoa au Wilaya;
“Kiongozi” maana yake ni mtu yeyote aliyepewa dhamana ya uongozi wa chama.
“Msajili” maana yake ni Msajili au Msajili msaidizi wa Vyama vya Michezo.
“Sheria” maana yake ni sheria namba 12 ya 1967
Utaratibu wa kusajili:
3.(I) Chama chochote kinachotaka kusajiliwa jitapeleka maombi yake kwa Msajili Msaidizi aliyeko katika wilaya ambayo ni makao makuu ya chama hicho. Maombi haya yaambatanishwe na:
(II) Baada ya kuwasilishwa maombi, Msajili Msaidizi atawapatia viongozi wa chama fomu Na. BMT 1 na BMT 2 wazijaze na kisha Msajili wa Vyama vya Michezo
(III) Msajili akishayapokea maombi hayo, atayahakiki na endapo hataona upungufu wowote, atakisajili chama hicho kwa kufanya yafuatayo:
(IV) Endapo Msajili atabaini upungufu kwenye maombi yaliyowasilishwa kwake na Msajili Msaidizi, atawajulisha wahusika upungufu uliopo kwa kutumia fomu Na. BMT 3 ili wakafanyie marekebisho.
(V) Endapo msajili atakataa kukisajili chama, atatoa taarifa kwa chama husika kwa kutumia Fomu Na .4 BMT
(VI) Chama cha mchezo wowote hakitaruhusiwa kuendesha shughuli za Michezo bila kusajiliwa. Aidha, chama kilichosajiliwa hakiruhusiwi kuwa na ushirikiano wa kimichezo na chama ambacho hakijasajiliwa.
4(I) Kila katiba ya chama inatakiwa kuonyesha kwa uwazi mamboyafuatayo:
Timu ya Taifa ya Kuogelea Tanzania iliyokuwa na jumla ya wan...
Tanzania imeandika historia mpya katika mchezo wa kikapu kwa...
Timu ya Taifa ya Wavulana chini ya umri wa miaka 15 (U15) in...
Shirikisho la Mchezo wa Karate Nchini Tanzania (TSKF) lime...
Timu za mpira wa mikono za Ngome kwa wanaume na wanawake zim...