FOX DIVAS YAANDIKA HISTORIA, YAFUZU FAINALI ZA VIL...

FOX DIVAS YAANDIKA HISTORIA, YAFUZU FAINALI ZA VILABU BINGWA AFRIKA KWA WANAWAKE

26 Oct, 2026
FOX DIVAS YAANDIKA HISTORIA, YAFUZU FAINALI ZA VILABU BINGWA AFRIKA KWA WANAWAKE

Tanzania imeandika historia mpya katika mchezo wa kikapu kwa upande wa vilabu vya wanawake baada ya timu ya Fox Divas kufuzu kwa mara ya kwanza kushiriki fainali za mashindano ya Vilabu Bingwa Afrika kwa Wanawake, zitakazofanyika mwezi Desemba jijini Cairo, Misri.

Fox Divas imefanikiwa kutinga hatua hiyo baada ya kuifunga timu kongwe ya KPA kutoka Kenya, ambayo ilikuwa mshiriki wa fainali za mwaka jana, kwa jumla ya vikapu 102-97, na hivyo kujihakikishia nafasi ya kuiwakilisha Tanzania katika mashindano hayo makubwa ya klabu barani Afrika.

Kwa matokeo hayo, Fox Divas itajiunga na timu za Rwanda, REG na APR, katika hatua ya fainali za mashindano hayo yatakayokutanisha vilabu bora vya wanawake barani Afrika.

Caption