Baraza la Michezo la Taifa (BMT) limeendesha mafunzo kwa Walimu wa Michezo mkoani Manyara, kwa lengo la kuwajengea uwezo na kuongeza ujuzi katika ufundishaji na uendelezaji wa michezo mashuleni.
Mafunzo hayo ni sehemu ya juhudi za BMT za kuimarisha michezo katika shule, kuibua vipaji na kukuza kizazi cha wanamichezo bora nchini.