MAGDALENA SHAURI AANDIKA HISTORIA CHICAGO MARATHON 2025.

Mwanariadha shupavu wa Tanzania, Magdalena Crispine Shauri, ametikisa dunia baada ya kuibuka na Medali ya Shaba katika mashindano ya kifahari ya Chicago Marathon 2025 yaliyofanyika nchini Marekani, akiboresha historia ya michezo ya riadha Tanzania!
Magdalena amekimbia kwa muda wa 2:18:03 (Personal Best), muda bora zaidi katika maisha yake ya ushindani na uliovunja rekodi ya Taifa ya Tanzania kwa mbio ndefu za Marathon kwa wanawake. Hii ni rekodi mpya inayoweka jina la Tanzania kwenye ramani ya dunia katika mchezo wa riadha.
Hii si mara ya kwanza kwa Magdalena kung’aa kimataifa!
Septemba 24, 2023, alishika tena nafasi ya tatu (3) kwenye Berlin Marathon nchini Ujerumani kwa muda wa 2:18:41, akiweka historia kama mmoja wa wanawake wa Kiafrika wanaopanda juu kwa kasi katika mbio ndefu duniani.
Hongera Magdalena Shauri!
Historia imeandikwa tena na jina lako litabaki kama alama ya fahari, uthubutu, na ubora wa mwanamke Mtanzania anayeng’ara duniani!