BMT yahitimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja kwa kuendelea kuwahudumia wadau mbalimbali

10 Oct, 2025
Baraza la Michezo la Taifa (BMT) limehitimisha maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja kwa mafanikio makubwa, likitoa huduma na elimu ya masuala mbalimbali kwa wadau wa michezo na wananchi waliotembelea ofisi za BMT zilizopo ndani ya Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam.
Katika maadhimisho hayo yaliyodumu kwa siku tano, Maafisa wa BMT wamewahudumia wadau wa michezo kutoka taasisi mbalimbali kwa kutoa elimu kuhusu majukumu yake, taratibu za usajili wa vyama vya michezo, utoaji wa vibali na namna bora ya uendeshaji wa shughuli za michezo nchini.