MSAJILI WA VYAMA VYA MICHEZO NCHINI AHITIMISHA KOZI YA WATAALAM WA TIBA MICHEZONI

10 Oct, 2025
Msajili wa Vyama vya Michezo Nchini, Bw. Abel M. Ngilangwa, amehitimisha rasmi kozi ya wataalam wa tiba michezoni iliyokuwa ikiendeshwa na Chama cha Madaktari wa Michezo Tanzania (TASMA) katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.
Kozi hiyo ya siku tano ilianza tarehe 6 na kuhitimishwa tarehe 10 Oktoba 2025 iliwashirikisha wataalam kutoka kada mbalimbali za sekta ya afya ikiwemo madaktari, wauguzi, wataalam wa mazoezi ya mwili, na wataalam wa lishe.
Kozi hiyo imehitimishwa kwa washiriki kupatiwa vyeti vya ushiriki, huku TASMA ikiahidi kuendeleza mafunzo kama hayo katika mikoa mingine nchini ili kuhakikisha kila eneo linakuwa na wataalam wa kutosha katika tiba michezoni.