UCHAGUZI WA VIONGOZI WA KAMISHENI YA NGUMI ZA KULIPWA TANZANIA (TPBRC)
20 Apr, 2023

Baraza la Michezo la Taifa (BMT) linapenda kuwataarifu wanachama na wadau wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBRC) kuwa, uchaguzi wa viongozi wa Kamisheni hiyo unatarajiwa kufanyika tarehe 13 Mei, 2023, jijini Dar es Salaam.

Fomu za kugombea nafasi tofauti katika uchaguzi huo zitaanza kutolewa katika Ofisi za BMT zilizopo Uwanja wa Benjamin Mkapa, kuanzia tarehe 12 Aprili hadi 10 Mei, 2023 lakini pia fomu zitapatikana katika tovuti ya Baraza la Michezo ambayo ni www.bmt.go.tz.

Aidha,usaili wa wagombea wa nafasi tofauti unatarajiwa kufanyika tarehe 12 Mei, 2023.