TANZANIA YAIBUKA BINGWA WA CAF SCHOOLS FOOTBALL CHAMPIONSHIPS CECAFA QUALIFIERS 2025
service image
10 Dec, 2025

Timu ya Taifa ya wasichana U15 imeandika historia baada ya kushinda Mashindano ya CAF African Schools Football Championships – CECAFA Qualifiers 2025, yaliyofanyika nchini Uganda

Tanzania waliibuka na ushindi kwa penati (5-4) dhidi ya Timu ya Taifa ya Ethiopia, matokeo yaliyowapa ubingwa wa mashindano hayo ya ukanda wa CECAFA. Ushindi huu unatambulisha Tanzania kama moja ya nguvu mpya za mpira wa miguu kwa shule katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

Pia Timu ya Taifa ya wasichana Under 15 yajizolea kitita cha Dola 100,000 kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kwa kutwaa ubingwa huo.