UCHAGUZI WA VIONGOZI WA CHAMA BAISKELI TANZANIA (CHABATA)
service image
20 Apr, 2023 10:00AM - 4:00PM DODOMA

Baraza la Michezo la Taifa (BMT) linapenda kuwatangazia wanachama na wadau Chama cha Baiskeli Tanzania (CHABATA) kuwa, uchaguzi wa viongozi wa Chama hicho uliokuwa ufanyike tarehe 02 Aprili, 2023 umesogezwa mbele hadi 07 Mei, 2023 jijini Dodoma.

Fomu za kugombea nafasi tofauti kwa mujibu wa katiba ya CHABATA zitaendelea kutolewa katika Ofisi za BMT na zinapatikana katika tovuti ya Baraza ambayo ni www.bmt.go.tz hadi tarehe 02 Mei, 2023.

Usaili wa nafasi hizo utafanyika tarehe 06/05/2023 siku moja (1) kabla ya kuelekea katika uchaguzi huo.

Nafasi zinazogombewa katika uchaguzi huo ni pamoja na:

           Nafasi                                                                            Ada

  1. Mwenyekiti                                                                     
  2. Mwenyekiti Msaidizi                                                        50,000/=
  3. Katibu Mkuu   
  4. Katibu Mkuu Msaidizi
  5. Wajumbe watano (5) wa kamati ya utendaji  -                30,000/=                                                                        

Sifa za wagombea   

  1. Awe na elimu ya Sekondari ya kidato cha nne au zaidi ya hapo,
  2. Awe na taaluma, uzoefu wa kuongoza na ujuzi wa mchezo wa baiskeli.
  3. Awe ni raia wa kuzaliwa wa Tanzania na mpenda michezo.
  4. Awe na nidhamu inayokubalika katika michezo na jamii kwa ujumla.

Malipo ya fomu yafanyike katika akaunti ya Baraza, kwa kutumia mfumo mpya wa malipo Serikalini.

Ili kupata namba ya utambulisho wa malipo mgombea anashauriwa kupiga namba za simu 0735 414043 au 0735 892889 kwa maelekezo zaidi.

Aidha, risiti ya malipo iwasilishwe Baraza pamoja na fomu zilizojazwa kwa usahihi na kuambatanishwa na nakala za nyaraka zote kulingana na sifa mahususi zilizoainishwa katika katiba ya chama hiki.

Hivyo Baraza linatoa wito kwa yeyote mwenye sifa kujitokeza kuchukua fomu kwa ajili ya uchaguzi huo na maendeleo ya Mchezo wa Baiskeli nchini.