BINGWA WA WBO NA WBC AWAPA SIRI YA MAFANIKIO MABONDIA WATANZANIA
service image
16 Aug, 2023

Bondia wa ngumi za kulipwa kutoka Uingereza ambaye ni bingwa wa Mikanda ya dunia WBO na WBC kutoka nchini Uingereza Natasha Jonas, amewaeleza mabondia wa Tanzania kuwa, kujiamini na kufanya kazi kwa bidii ndio Siri kubwa ya kufikia ndoto za mafanikio katika mchezo huo.

Amewaeleza hayo leo Agosti 16, 2023 katika kikao na mabondia wakulipwa na wangumi za wazi kilichoratibiwa na Baraza la Michezo la Tiafa (BMT) katika ukumbi wa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Natasha amesema kuwa, atakwenda kuzungumza na wadau wa mchezo huo nchini Uingereza Ili kuona namna gani watasaidia mabondia wa Tanzania kufika malengo yao.

"Katika hili nitatumia mawasilino ya nchini Uingereza na hapa Tanzania kusaidia ngumi kwa kufanya ushirikiana pamoja na elimu ya mchezo huu,"amesema Natasha.

Awali kwa niaba ya Katibu Mtendaji wa BMT Benson Chacha amemwomba Natasha kushirikiana na Mabondia wa Tanzania kwa kuandaa mapambano ili waendelee kuongeza ujuzi na kujiaamini.