DKT. SERERA NA WAJUMBE WAKE WATETA NA TEMBO WARRIORS.
service image
18 May, 2024

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo na Mkuu wa Msafara katika safari ya Misri kuipa nguvu timu ya Taifa ya Mpira wa miguu kwa watu wenye Ulemavu (Tembo Warriors) leo Mei 18, 2024 na ujumbe wake wameitembelea kambini timu hiyo na kuipa salamu za Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu na Watanzania wote kuhusu kiu yao.

"Kiu ya Dkt. Samia na Watanzania ni kuona mnajituma uwanjani na kuipa heshima nchi katika mashindano haya ya Afrika (AAFCON)".

Dkt. Serera katika safari hiyo ameambatana na Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bi. Neema Msitha, Mjumbe wa Baraza Maulid Mtulia, Wajumbe wa hamasa kwa Timu za Taifa Hamisi Ally na Mwanahabari Mkongwe Jemedari Said Kazumari.

Katika Ziara hiyo kambini hapo Cairo Misri Kila mjumbe ametoa wito wake wenye kuipa hamasa ya mafanikio timu hiyo, huku kwa upande Kocha Salvatori Edward na Nahodha wa timu hiyo Juma Kidevu wamewatoa hofu wajumbe hao na Watanzania na kuwaomba wawe nao katika maombi na Dua ushindi upo.