KATIBU MKUU YAKUBU ASHUHUDIA MECHI YA UFUNGUZI CECAFA
Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamduni, Sanaa na Michezo Saidi Yakubu amekuwa shuhuda wa mechi ya ufunguzi wa mashindano ya Mashirikisho ya Mpira wa Miguu ya nchi wanachama wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la nchi za Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kati ya Tanzania na Burundi katika uwanja wa Azam Compelex Chamazi Julai 25, 2023.
Hadi kipenga cha mwisho, timu ya Wasichana U-18 ya Tanzania imeibuka kidedea kwa kuwafunga wapinzani wao Burundi kwa magoli 3-0 ikiwa ni mechi ya ufunguzi wa michuano CECAFA.
Magoli ya Tanzania yamefungwa na Winfrida Gerald jezi Na 7 ambaye alifunga goli la kwanza, Sarah Joel jezi Na 19 alifunga goli la pili huku goli la tatu likifungwa na Aisha Juma jezi Na 9.
Katibu Mkuu katika klufunguzi huo aliambatana na Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bi. Neema Msitha.