KIKAO CHA PAMOJA NA JICA
service image
05 Jul, 2023

Baraza la Michezo la Taifa (BMT) katika kuendeleza ushirikiano baina yao na Shirika la Ushirikiano la Kimataifa la Japani (JICA) wameendelea kuwa na vikao vya mara kwa mara kujadili mambo tofauti ya kushirikiana katika kuendeleza michezo nchini.

Leo Agosti 4, 2023, Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Neema Msitha amekutana na Mwakilishi Mkuu wa JICA Bw. ARA Hitoshi aliyeambatana na watendaji wengine wa JICA Tanzania ambapo wamejadili mambo mengi ikiwemo mashindano ya riadha ya wanawake (Ladies First) kwa mwaka 2023.

Kikao hicho kimefanyika katika ofisi ya Katibu Mtendaji wa BMT iliyopo uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.