LIGI TAIFA WAVU YAZIDI KUSHIKA KASI
28 Jul, 2023
Mzunguko wa pili wa ligi ya taifa ya mpira wa wavu imeendelea kushika kasi kwenye viwanja vya Gwambina jijini Dar es salaam leo 28 julai, 2023.
Mzunguko huo ni wa lala salama kupata timu zitakazofuzu hatua ya robo fainali na zitakazoaga ligi hiyo kwa msimu wa mwaka huu.
Matokeo ya wanawake leo timu ya JKT iliishinda Magereza kwa seti 3-2 huku Mafinga Parish ilikubali kichapo kichapo cha seti 3-0 dhidi ya Jeshi Stars.
kwa upande wa wanaume JKT alishinda kwa seti 3-0 dhidi ya NHIF.
Ligi hiyo itaendelea kesho kwa michezo tisa kuchezwa kwenye uwanja huo.