MAAGIZO KWA KAIMU MKURUGENZI
service image
21 Sep, 2022

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mohamed Mchengerwa amemtaka Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Ally Mayay kuchapa kazi ili kuhakikisha michezo inapiga hatua ikiwemo kuhakikisha miundombinu inaboreshwa na kuwepo kwa taarifa za kina za wataalam wa michezo.

Aidha, amemtaka Mkurugenzi huyo kwa kushirikiana na Mtendaji Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Neema Msitha kuhakikisha vipaji vya wanamichezo tofauti vinaibuliwa kutoka katika ngazi ya chini ili taifa liweze kuwa na wanamichezo wengi wenye viwango.



Rai hiyo ameitoa leo Septemba 21 wakati wa hafla ya kuiaga na kuikabidhi bendera, vifaa vya Michezo na bima timu ya mpira wa miguu ya umri wa chini ya miaka 17 (U 17) watakaondoka Septemba 25 kuelekea katika kambi yao ya mwisho nchini Uingereza kabla ya kuelekea nchini India mwezi Oktoba kulipambania taifa katika kombe la dunia.

"Tumechoka kuitwa kichwa chawendawazimu nendeni mkajitume, mkapambane na muwe wazalendo kwa nchi yetu mrudi na kombe,"alisema Mhe. Mchengerwa.