MANYARA YAIBUKA BINGWA WA JUMLA WA LADIES FIRST 2025
30 Nov, 2025
Mkoa wa Manyara umeibuka mshindi wa jumla katika Mashindano ya Riadha ya Wanawake Ladies First 2025, baada ya kung’ara na kujikusanyia jumla ya medali nane (8). Kati ya hizo, tatu ni za dhahabu, mbili za fedha na tatu za shaba, hatua iliyowapa nafasi ya kuwa bingwa wa jumla wa mashindano ya msimu wa saba wa mashindano ya Ladies First.
Nafasi ya pili imechukuliwa na Mkoa wa Mjini Magharibi, ambao umejipatia medali sita (6) tatu za dhahabu, moja ya fedha, na mbili za shaba.
Kwa upande mwingine, Mkoa wa Kilimanjaro umeibuka nafasi ya tatu baada ya kupata jumla ya medali tatu (3), zikiwemo moja ya dhahabu na mbili za fedha.

