MASHINDANO YA KRIKETI AFRIKA MASHARIKI
service image
19 Aug, 2023

Timu ya Taifa ya Tanzania ya mchezo wa kricketi inatarajiwa kuondoka Tanzania kwenda nchini Rwanda kushiriki mashindano ya Afrika Mashariki yatakayoanza tarehe 20 Agosti, 2023.

Timu hiyo inatarajiwa kuondoka ikiwa na ujumbe wa watu 18 kushiriki michuano hiyo itakayoshirikisha mataifa 3 ambapo kila timu inatarajiwa kucheza michezo 12

Akizungumza kwenye hafla ya kukabidhiwa bendera ya Taifa hii leo Agosti 18, 2023 Afisa Michezo kutoka Baraza la Michezo la Taifa Nicholas Mihayo ameeleza kwamba BMT wanajivunia kufanya kazi na Chama cha kricketi Tanzania na wana matumaini kwamba timu hiyo itaendelea kufanya vizuri kama ambavyo imekuwa ikifanya miaka yote

Mihayo pia ameeleza kwamba serikali kupitia Wizara ya Michezo wanafanyia kazi maombi ya Chama hicho kuhusu kupata maeneo ya kuchezea mchezo wa kriketi nchini huku nahodha wa timu hiyo akiahidi kwamba wanaenda kupambana kwa ajili ya kuhakikisha timu inapata ushindi kwa heshima yao kama wachezaji na taifa kiujumla