MASHINDANO YA MUUNGANO MPIRA WA MIKONO
service image
02 May, 2023

Mashindano ya Muungano ya mpira wa mikono yamefunguliwa leo tarehe 2 Mei, 2023 kwa michezo miwili kupigwa kwenye Uwanja wa 95KJ.

Timu ya wanaume ngome imeibuka na ushindi wa magoli 35_24 dhidi ya Magnus, huku Kwa upande wa wanawake ngome ikikubali kichapo cha magoli 17 _11 dhidi ya JKT.

Mashindano hayo yataendelea kesho kwa kushuhudiwa michuano ya timu mbalimbali.

 

Mashindano hayo yameshirikisha timu tisa za wanawake na wanaume kutoka Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar ambapo yatahitimishwa Mei 05, 2023 Jijini Dar es salaam.