MHE. MCHENGERWA AKAGUA VIFAA VYA KISASA VYA MAZOEZI BENJAMIN
26 Mar, 2022
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohammed Mchengerwa, leo Jumamosi, Machi 26, 2022, ametembelea na kukagua ujenzi wa chumba maalum cha mazoezi ya viungo (gym), mradi ukiotekelezwa na Wizara hiyo ikiwa ni mwendelezo wa maboresho ya Uwanja wa Benjamin Mkapa. Tangu uwanja huo ukamilike mwaka 2007, hapakuwahi kuwa na chumba cha mazoezi chenye vifaa hivyo vya kisasa.