MIKAKATI YA MAENDELEO YA MICHEZO
service image
18 Apr, 2023

Kamati ya ufundi ya Baraza la Michezo la Taifa (BMT) leo Aprili 18, 2023 imekutana na kujadili mambo mbalimbali ya kuinua michezo ikiwemo uendelezaji wa miundombinu ya michezo samabamba na uwepo wa wataalamu wa michezo wenye sifa stahiki katika kila mchezo kwa maendeleo ya sekta hii nchini.

Kamati hiyo inaongozwa na Mwenyekiti ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Ally Mayay, Katibu wake Halima Bushiri Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Michezo wa Baraza pamoja na wajumbe Tuma Dandi, Dkt. Dovetha Marwa Mhadhiri Chuo Kikuu cha Dar es salaam na Ameir Mohammed Kamishna wa Michezo Zanzibar.