MIPANGO, SERENGETI WAANZA KWA KISHINDO WAVU TAIFA
service image
21 Sep, 2022

Timu ya Mipango, Serengeti zimeanza kwa kishindo kwa kuibuka na ushindi katika michezo yao ya mzunguko wa pili wa Ligi ya Taifa ya mchezo wa wavu ambao umeanza Septemba 20 kwenye Uwanja wa Ndani wa Taifa Dar Es Salaam.



Mipango imeanza kwa kuibuka kwa seti 3_0 dhidi ya Kigamboni huku
Serengeti ikiwapigisha gwaride Maafande wa Nyika kwa seti 3_2.

Matokeo mengine Faru imekubali kichapo cha seti 3_0 dhidi ya Chui, wakati KIUT imeshinda kwa seti 3_0 dhidi ya HVC.

Aidha Tanesco imepokea dozi ya seti 3_0 dhidi ya NHIF, huku mtanange wa mwisho Jeshi Star imeshinda seti 3_1.

Akizungumza wakati wa michuano hiyo Kocha wa Mipango Dickson Dick, amesema mazoezi, kujituma ndio siri ya kuibuka na ushindi huo.

Amesema ushindi huo umewapa na molari na ari ya kuhakikisha wanajipanga kupata matokeo mazuri katika michezo ya makundi.

"Mzunguko wa kwanza tulikuwa wageni na tulirudi nyumbani kujipanga, na huu mchezo wa kisasi mzunguko wa kwanza walitufunga seti 3_0 na sisi leo tumerudisha kwa kuwafunga seti 3_0," amesema Dick.