MSITHA: MUDA SI MREFU CHANGAMOTO YA USAJILI ITAPATIWA SULUHISHO
service image
27 Oct, 2022

Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Neema Msitha ameeleza kuwa, changamoto ya usajili muda sio mrefu itapatiwa suluhisho la kudumu huku akithibitisha kuwa utaratibu wa kuwa na mfumo wa usajili kidijitali uko kwenye hatua nzuri.

Aidha, ameongeza kuwa, changamoto hiyo ilitokana na kukosekana kwa msajili kwa muda kidogo na kusema kuwa kwa sasa BMT imekamilika kwa kuwa msajili wa vyama vya michezo yupo, na kuwataka wadau kutokuwa na wasiwasi kuhusu kusajiliwa.

Msitha amethibitisha hayo leo wakati wa uzinduzi wa programu ya kuwahamasisha na kuwaendeleza wanawake na wasichana katika soka ijulikanayo kwa jina la 'Mpira Fursa' iliyoanzishwa na Taasisi ya Karibu Tanzania (KTO) inayomilikiwa na Mwanahabari Magid Mjengwa.

"Nawapongeza sana (KTO) kwa kazi kubwa wanayofanya ambayo tulitakiwa kuifanya sisi BMT, Wizara na TFF,"alisema Msitha