BMT WAUNGANA NA MAMA MARIA NYERERE KUTOA BARAKA KWA WAENDESHA BAISKELI
service image
01 Oct, 2023

Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kama wasimamizi wa michezo nchini leo Oktoba Mosi, 2023 wameungana na Mama Mama Maria Nyerere kutoa Baraka kwa Waendesha baiskeli wa twende Butiama ambao wameanza safari ya kuekekea butiama.

Lengo la msafara huo ni kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere likiwa na waendesha baiskeli kutoka Tanzania, Kenya, Malawi, Rwanda na Congo.

Msafara huo umeanzia Dar es Salaam ambao utapita Mikoa 10 na Wilaya 20 za Tanzania bara ukikusudia kuhitimishwa butiama tarehe 14 Oktoba 2023 siku ya kumbukizi ya kifo cha Baba wa Taifa.