KATIBU MKUU MSINGWA ATOA KONGOLE KWA IKANGAA
service image
25 Nov, 2023

Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Gerson Msigwa ametoa pongezi kwa mwanariadha mkongwe, Kanali Mstaafu Juma Ikangaa kwa kufanya uamuzi wa busara kutafuta udhamini wa kushindanisha wanariadha wa kike akiamini Tanzania Kuna vipaji vingi vya riadha.

Aliongeza kuwa mipango yao kwa mwakani mashindano hayo ni kuyafanya yawe makubwa zaidi ya mwaka huu na kuleta matokeo makubwa.

"Tumepokea maelekezo ya Waziri ya kujiandaa kufanya mashindano hayo kwa ukubwa zaidi, na tungeomba JICA kuongeza bajeti hata mara tano zaidi, Ili mwakani liwe tukio kubwa litakalotikisa nchi nzima," alisema Msigwa.