MSIMU WA SABA WA LAIDIES FIRST
service image
26 Nov, 2025

Msimu wa saba wa Mashindano ya Riadha ya Wanawake utafanyika Novemba 28–30, 2025 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam. Mashindano hayo yatafanyika Novemba 29–30, yakitanguliwa na semina kwa wanariadha na waamuzi Novemba 28.

Akizungumza Novemba 26, 2025, Katibu Mtendaji wa BMT, Bi. Neema Msitha, amesema maandalizi yamekamilika na mgeni rasmi atakuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Palamagamba Kabudi, sambamba na uwepo wa viongozi kutoka Japan, JICA, AT na taasisi nyingine.

Jumla ya wanariadha 155 kutoka mikoa 31 ya Tanzania Bara na Zanzibar watashindana katika mbio mbalimbali ikiwemo 100m, 200m, 400m, 800m, 1500m, 5000m, 4×100m pamoja na kurusha mkuki. Tukio hilo litaambatana na mafunzo ya matumizi ya taulo za kike, nidhamu ya fedha na upimaji wa afya.

BMT imemshukuru Kanali mstaafu Jumaa Ikangaa kwa kuanzisha mashindano haya kwa ushirikiano na JICA, ambayo yamekuwa chachu ya kukuza vipaji vya wanariadha wa kike. Wakazi wa Dar es Salaam wametakiwa kujitokeza kwa wingi kutoa hamasa kwa washiriki.