TAMASHA LA MICHEZO KWA WOTE, MKINGA
02 Dec, 2025
Tamasha la Michezo kwa Wote, linaloratibiwa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kwa ushirikiano na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA), linatarajiwa kuendelea kufanyika leo Disemba 3, 2025 katika viwanja vya Shule ya Msingi Kasera, wilayani Mkinga mkoani Tanga.
Tamasha hili pia linatarajiwa kuibua vipaji vipya na kuongeza ari ya ushiriki wa michezo shuleni na katika ngazi za jamii, hivyo kuchangia juhudi za serikali katika kukuza sekta ya michezo nchini.

