TANZANIA, KENYA NA UGANDA WAPO TAYARI AFCON 2027
31 Jul, 2023
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amesema Serikali ya Tanzania ipo tayari kuandaa michuano hiyo pamoja na Kenya na Uganda kwa kuwa uamuzi huo umefanyiwa kazi katika ngazi ya juu ya serikali.
Hayo ameyasema tarehe 30 Julai, 2027 wakati akifungua kikao cha kuwakaribisha wataalam kutoka Shirikisho la mpira wa miguu Afrika (CAF) waliofika nchini kwa ajili ya kukagua miundombinu ya michezo kwa ajili ya utayari wa Tanzania, Uganda na Kenya kuwa wenyeji wa Afcon 2027.