TANZANIA MABINGWA U-18 CECAFA
service image
05 Jul, 2023

TIMU ya Taifa ya Tanzania ya Wasichana U-18 wamefanikiwa kutwaa ubingwa wa mashindano ya kuwania ubingwa kwa Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati CECAFA.

Tanzania imetwaa ubingwa huo baada ya kuibuka na ushundi wa bao 1-0 dhidi ya Uganda katika mchezo uliopigwa jana 4 Agosti, 2023 kwenye uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es Salaam.



Bao la Tanzania limefungwa na mchezaji wake Winfrida Gerald dakika ya 43.

Tanzania ni wenyeji wa michuano hiyo ikivuna pointi 10 wakiongoza msimamo wa michuano hiyo iliyoendeshwa kwa mtindo wa ligi huku Uganda wakishika nafasi ya pili kwa alama 9.

Nafasi ya tatu ikishikiliwa na Ethiopia akiwa na alama sita, Burundi akishika nafasi ya nne akiwa na pointi tatu na Zanzibar ikishika mkia baada ya kupoteza mechi zote.