WATANZANIA WAITWA KUSHIRIKI MCHEZO WA GOFU
service image
01 Oct, 2023

Kufuatia kukua na kuenea kwa mchezo wa Gofu katika maeneo mbalimbali nchini, Watanzania wameitwa kujitokeza kushiriki mchezo huo ili kunufaika na fursa zinazopatikana hususani katika Mashindano makubwa yanayoandaliwa ndani na nje ya nchi.

Wito huo umetolewa na Bakari Machumu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communication Limited ambaye alikuwa mgeni rasmi katika halfa ya utoaji zawadi za washindi wa Shindano la gofu la NCBA Golf Series yalikuwa yanafanyika katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar Es Salaam, huku akifurahishwa na ushindani wa mchezo huo na kuwataka Watanzania kujitokeza kushiriki gofu

Kwa upande wa Wadhamini wa Shindano hilo Benki ya NCBA wameeleza kufurahishwa na Shindano la mwaka huu na kuwashukuru wote waliofanikisha mchezo huo kukua zaidi.