UKARABATI WA UWANJA WA BENJAMIN MKAPA
service image
27 Jul, 2023

Balozi Dkt. Pindi Chana Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo leo Julai 27, 2023 amepokea picha ya mfano ya benchi la ufundi na wachezaji wa ziada kutoka Makamu wa kwanza wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Athuman Nyamlani, litakalojengwa na Shirikisho hilo katika Uwanja wa Benjamin wakati wa ukarabati mkubwa wa Uwanja huo unaotarajiwa kufanyika hadi Julai 2024.