UKARABATI WA UWANJA WA MKAPA
service image
08 Aug, 2023

Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Saidi Yakubu amesema, ukarabati wa awali wa Uwanja wa Mkapa utajumuisha masuala mbalimbali ambayo CAF wanahitaji yafanyiwe kazi mapema, baadhi ya maeneo yanagharamiwa na CAF wenyewe ikiwa ni sehemu ya mkataba kwa ajili ya mechi hiyo ya ufunguzi ambayo itafanyika nchini.

Kwa hivi sasa mpaka Oktoba 20, 2023 hakutakuwa na mechi nyingine itakayochezwa kwenye uwanja huu wa Benjamin Mkapa ili kupisha maandalizi kwa sababu miongoni mwa vitu watakavyofanya African Football League ni pamoja na kufumua eneo la kuchezea mpira kwa gharama zao na watalirejesha kwenye hali ambayo unachezeka mpira.

Haya ameyasema leo Agosti 08, 2023 baada ya kuupitisha ujumbe kutoka CAF kwenye baadhi ya maeneo muhimu ya uwanja huo ikiwa ni maandalizi ya ligi ya timu nane za Afrika Simba ikiwa ni mwakilishi wa timu kutoka Afrika Mashariki.