VETERANS MARATHON KUWAENZI WACHEZAJI WA ZAMANI WA MPIRA WA MIGUU
service image
18 Apr, 2023

Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Neema Msitha, amekutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Umoja wa wachezaji wa zamani wa Mpira wa Miguu Tanzania UMSOTA, kujadili namna ya kuandaa matukio mbalimbali ya kimichezo kama vile 'Marathon', ili kuwaenzi wachezaji hao nchini.

Msitha amekutana na wachezaji hao leo tarehe 18 Aprili, 2023 Ofisini kwake uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam.

Wachezaji walioshiriki katika kikao hicho ni pamoja na Mwenyekiti Faza Lusozi pamoja na Jamal Lwambo.