VIPAJI VYA SOKA YA WANAWAKE VYAENDELEA KUIBULIWA
service image
20 Aug, 2023

Serikali ya Sweden kupitia Ubalozi wake nchini Tanzania umefanya hafla ya kuadhimisha miaka 60 ya ushirikiano baina ya mataifa hayo ambapo miongoni mwa shughuli nyingi, umefanyika mchezo wa kirafiki baina ya timu za watoto wa kike kutoka Shule ya Msingi ya Uhuru.



Akizungumza wakati wa hafla hiyo akimuwakilisha Katibu mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa,jana Agosti 18, 2023 Afisa Michezo wa BMT Charles Maguzu ametoa pongezi kwa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) kwa kuendeleza programu za kuinua michezo ya wanawake nchini na matunda ya programu hizo yameonekana kupitia timu za wanawake za Tanzania

Ameishukuru Serikali ya Sweden kupitia Ubalozi wake nchini kwa kuendeleza ushirikiano na Serikali ya Tanzania kwenye kuendeleza michezo ya watoto wa kike ikiwa sehemu ya kuendeleza soka la wanawake Pia ameiomba Serikali ya sweden kufadhili masomo ya makocha wa tanzania kwenda sweden kupata mafunzo ya muda mrefu na muda mfupi ili kupata wataalamu wengi

Ameahidi kwamba serikali ya Tanzania ipo tayari kushirikiana na serikali ya Sweden na TFF kwenye programu mbalimbali za kuendeleza soka la wanawake nchini Tanzania kwani Taifa la Sweden ni miongoni mwa mataifa yaliyofanikiwa kwenye soka la wanawake.