PROGRAMU YA UTOAJI WA TUZO ZA WANAMICHEZO BORA WA MWAKA
1.0 Utangulizi
Baraza la Michezo la Taifa (BMT) limekuwa na jukumu la msingi la kukuza na kuendeleza michezo kwa kushirikiana na vyama na mashirikisho ya michezo ya kitaifa nchini. Baraza limekuwa na mikakati mbalimbali ya kuchochea maendeleo ya michezo mojawapo ya mkakati wa Baraza ni utoaji wa tuzo za wanamichezo wanaofanya vizuri kwa kila mwaka kwenye mashindano ya michezo mbalimbali ya kitaifa
2.0 Lengo
Baraza limeweza kUratibu utoaji wa tuzo kwa wanamichezo waliofanya vizuri kwa misimu mitatu mfululizo ili kusherekea mafanikio ya timu na wanamichezo wetu katika mashindano ya kimataifa na kitaifa. Tuzo hizo zimetumika kama kichocheo kikubwa cha mafanikio haya makubwa yanayoonekana katika sekta ya michezo nchini.
2.1 Malengo Mahsusi ya Tuzo
3.0 Uratibu na Usimamizi wa Tuzo
Shughuli hii ya utoaji wa tuzo inaratibiwa na kusimamiwa na;
4.0 Vipengele vya Tuzo
Baraza limekuwa likifanya kazi kwa ukaribu sana na Vyama na mashirikisho ya michezo ya kitaifa katika kuwatambua wanamichezo na timu zilizofanya vizuri katika tasnia ya michezo. Vyama/mashirikisho vinaandikiwa barua na kupewa fomu maalumu ili kuwasilisha majina ya wachezaji, viongozi, wataalaumu na timu zilizofanya vizuri na kupitiwa na Sekretarieti na baadaye kuthibitishwa na Kamati ya usimamizi. Vipengele vya tuzo ni kama ifuatavyo;
5.0 Faida za Tuzo
6.0 Tarehe ya Utoaji Tuzo na Mgeni Rasmi
Kamati wa usimamizi na uratibu wa utoaji tuzo za wanamichezo bora upanga tarehe ya tukio, ambayo huwa usiku na mmoja ambapo wanamichezo wote waliopendekezwa na kamati wanakutana na kusherekea siku hiyo kwa namna ya kipekee. Pia wageni mbalimbali wa Serikali na taasisi za michezo hualikwa kujumuika pamoja kusherekea usiku wa tuzo za wanamichezo bora. Kamati upendekeza jina la mgeni rasmi kutoka Serikalini.
7.0 WAGHARAMIAJI WA TUZO, NA WAFADHILI
Shughuli ya tuzo kwa wanamichezo bora imekuwa ikigharamiwa na Serikali kwa kushirikiana, wafadhili na wadhamini mbalimbali.
PROGRAMU YA UENDELEZAJI UTAWALA BORA KATIKA VYAMA NA MASHIRIKISHO YA MICHEZO...
PROGRAMU YA MASHINDANO YA “LADIES FIRST Mashindano ya Riadha ya Wanawak...
TAMASHA LA MICHEZO LA WANAWAKE Utangulizi Tamasha la Michezo kwa wana...